Siku ya kesho katika jiji la London pande zake za Magharibi katika kitongoji cha Fulham pale darajani maarufu kama Stamford Bridge mashabiki zaidi ya elfu 40 wanategemewa kuujaza uwanja huo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza. Nami kama kawaida yangu nakuletea habari zote kuhusu mechi zinazochezwa.
Tunaanza kama kawaida
Chelsea na Swansea mara ya kwanza kukutana ilikuwa tarehe 21-November-1925 katika dimba la Stamford Bridge ambapo kwa siku hiyo mashabiki 43827 walikuwa uwanjani kuangalia pambano hilo lililoisha kwa The Blues kupoteza kwa mabao 3-1. Bao pekee la Chelsea likifungwa na Hilding. Ambapo Swansea walikuwa wakiitwa Swansea Town.
Na mara ya mwisho kukutana kwa timu hizo ilikuwa 11-September-2016 katika dimba la Liberty Stadium uwanja wa unaotumiwa na Swansea. Na siku hiyo uwanja huo uliingiza jumla ya mashabiki 20865 na mchezo huo kuisha kwa sare ya 2-2. Magoli ya Swansea yalifungwa na Fer pamoja na Sigurdsson na huku kwa upande wa Chelsea yakifungwa na Diego Costa yote mawili.
Mchezo ambao ulishudiwa kuingiza magoli mengi ilikuwa Chelsea ameshinda magoli 6-1.
Mchezo wa kesho unategemewa kuwa na utamu mwingi, ila haya ndio baadhi;
1. Makocha bora kupambana, Antonio Conte aliyeshinda tunzo ya kocha bora mara tatu mfululizo dhidi ya Paul Clement aliyetwaa ukocha bora wa mwezi January.
2. Veterani Claude Makelele kurudi darajani kama kocha. Aliichezea Chelsea na kuipatia mafanikio makubwa na safari hii anarudi Chelsea akiwa kama kocha msaidizi wa Swansea.
3. Lampard kusalimia mashabiki akiwa uwanjani. Tangu aondoke Chelsea amekuwa akija anaangalia mechi akiwa jukwaani tu lakini siku ya kesho inategemewa atakuwepo uwanjani na atawasalimia mashabiki. Anaweza akapewa kibarua cha kuwa balozi wa Chelsea.
4. Conte kukutana tena na Llorente. Antonio Conte ambaye alishawai kufanya kazi na Llorente ambapo ni mchezaji wa Swanse kesho watakutana tena.
5. Utamu wa mechi, Chelsea atataka ashinde ili kutengeneza tofauti kubwa kati yake na anayemfata wakati Swansea watataka ushindi ili kutoka kwenye nafasi ya kushuka daraja.
No comments:
Post a Comment