Kinda anayetajwa kuwa na kipaji cha hali ya juu alielelewa kwa muda mrefu ndani ya Chelsea academy akitokea timu ya vijana ya Anderlecht iliyopo Ubelgiji, Charly Musonda au mwenyewe anajiita Musonda Jr. ambaye ni mchezaji halali wa Chelsea ingawa kwa sasa anakipiga Real Betis ya Hispania ametoa tahadhari kwa akina Willian na Pedro.
Charly Musonda ambaye pia yupo karibu na mdogo wa Eden Hazard aitwaye Thorgan Hazard amekuwa akimwambia sana Thorgan kwamba msimu ujao anarudi Chelsea lakini kurudi kwake anarudi kuja kufanya kazi na kwa maana hiyo wale wanaocheza nafasi moja na anayocheza yeye wajiandae.
Musonda Jr. aliezaliwa mwaka 1996 mwezi wa 10 ameonekana kuwa mwendelezo wa kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji, ambapo chenga zake na uwezo wake uwanjani umekuwa ukiwatoa denda mascout wa timu mbalimbali ingawa yeye amekuwa akisisitiza kwamba bado anataka kurudi Chelsea.
No comments:
Post a Comment