Wednesday 8 February 2017

Morata ndani, Costa nje?

Ndilo swali ambalo bado linatawala katika vichwa vya wengi kwa wachambuzi na hata wapenda soka kwa sasa.

Mshambuliaji anayeongoza kwa magoli kwa sasa ndani ya klabu ya Chelsea, Diego Costa amekuwa akiendelea kuhusishwa kwamba haonekani kama ana muda mrefu ndani ya klabu hiyo yenye makao yake kusini mwa jiji la London.

Japo kulikuwa na taarifa za yeye kuhusishwa na ofa ya kununuliwa na klabu ya Tianjin Quanjin ya nchini China wakati wa dirisha dogo la usajili lakini mpaka dirisha hilo linafungwa alibaki Chelsea ambapo pia kocha wake Antonio Conte hakuwa tayari kumuuza.

Lakini sasa habari zinaonekana kupamba moto huku mwenyewe Costa akionekana kutokuwa na furaha tena ndani ya Uingereza na akishinikiza auzwe.

Wakati hayo yakitokea Alvaro Morata ambaye pia ni mhispania ambaye kwa sasa anachezea Real Madrid ndie ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Diego Costa.

Alvaro Morata ambaye pia alishawai kuwa chini ya kocha wa sasa wa The Blues anaonekana kutajwa sana kujiunga na Chelsea. Ikumbukwe, kabla ya Morata kurudi timu yake ya zamani ya Real Madrid akitokea Juventus, Chelsea walishaonyesha nia ya kumtaka naye alishakili kwamba Chelsea walimwekea £60 Milioni (paundi milioni 60)

Alvaro Morata tangu arudi Real Madrid amekuwa hana uhakika wa namba japo amekuwa na uwiano mzuri wa kufunga. Akiwa na magoli 6 akiwa ameyafunga kwa dakika 668 ambazo ni sawa na kufunga goli 1 kwa kila baada ya dakika 110.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.