Friday, 17 February 2017

Mashabiki kuandamana Sanchez aondoke Arsenal

Wananchi wa Chile ambayo ni nchi aliyozaliwa mchezaji nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez wamepanga kuandamana ili kuweza kumshawishi nyota wa huyo aweze kuachana na Arsenal. Mashabiki hao ambao walijiunga kama kampeni katika mtandao wa Facebook wakiwa na agenda ya kuandamana katika jiji alilozaliwa mchezaji huyo ili kumshawishi Sanchez ahame Arsenal kwa kuwa wamechoka kumuona anadhalilika akiwa na timu hiyo baada ya kushuhudiwa timu ya Arsenal ikichakazwa na Bayern Munich katika mchezo wa Uefa kwa goli 5-1 huku Sanchez akiwemo ndani. Lakini pia inasemekana mchezaji huyo hakuwa na furaha walipokuwa kwenye vyumba vya kubadilushia nguo baada ya mchezo huo.

Najua utajiuliza kwanini nimeiweka habari hii katika blog ya Chelsea.
Jibu ni kwamba hii ni kama itachochea ama kuongeza nguvu kwa Chelsea maana walikuwa wanatajwa kuwa na mpango wa kumsajili timu hiyo.

Sasa hapo ni kama viongozi wa Chelsea wakitulia na kuwa nae vizuri wanaweza wakamnyakua na msimu ujao akavaa jezi ya Chelsea ikiwa imetengenezwa na kampuni ya Nike.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.