Kuelekea mchezo wa jumamosi ya tarehe 18-February katika kombe la FA kati ya Wolves dhidi ya Chelsea leo nakuletea historia zao kabla ya kukutana tena hapo jumamosi.
Wamekutana mara 106 katika michuano yote na katika michezo hiyo Chelsea wameshinda michezo 40 na kufungwa 38 na uku wakitoka sare michezo 26.
Mara ya kwanza timu hizo kukutana ilikuwa mwezi December mwaka 1906 katika ligi daraja la pili na Chelsea wakashinda kwa goli 2-1.
Wakati mara ya mwisho kukutana ilikuwa mwaka 2012 na Chelsea walitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 6-0 ambapo magoli yalifungwa na Gary Cahill, Oriol Romeu, Juan Mata, Victor Mosess, Ryan Betrand na Fernando Torress.
No comments:
Post a Comment