Thursday 9 February 2017

Costa & Courtois hali bado tete

Mpaka sasa hali ni tete ndani ya Chelsea. Mpaka sasa haijajulikana itakuwaje kwa wachezaji wake nyota Diego Costa na Thibaut Courtois baada ya wote kubakiza miaka 2 katika mikataba yao.

Atletico Madrid bado wana nia na wanaendelea kutaka kama Diego Costa arudi kwenye timu yao baada ya kumuuza misimu miwili iliyopita. Mchezaji huyo ambaye amekuwa akihusishwa na fununu za kuhama klabuni hapo ambapo kama hiyo haitoshi amekuwa akikaririwa akisema hana furaha tena Uingereza na haswa akivishutumu vyombo vya habari vya nchini hapo havimpendi na vinamfatilia sana.

Wakati huo pia mabingwa wa zaidi ya mara 10 wa kombe la klabu bingwa ya dunia, Real Madrid wamekuwa wakihusishwa kwa karibu na nia yao ya kumsajili Thibaut Courtois ambaye naye pia aliwai kukiri furaha yake iliisha siku ile tu alipoondoka Hispania ambapo alikuwa kwa mkopo katika klabu mahasimu wa Real Madrid klabu ya Atletico Madrid. Ambapo Real Madrid wamekuwa wakimtafuta mbadala wa kipa mzuri tangu Iker Casillas aondoke klabuni hapo lakini pia wanamtaka kipa wa Man utd, David De Gea.

Nadhani Chelsea inapaswa kuwaongezea mkataba wachezaji hawa kwa kuwa bado inawahitaji haswa kwa kipa Courtois ambaye amekuwa na kiwango kizuri haswa msimu huu akiwa ameruhusu kufungwa mabao 16 tu, na kuwa na Cleansheet zaidi ya 13.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.