Friday 30 September 2016

Conte apata majanga

Antonio Conte amepata pigo kuelekea mechi ya jumamosi dhidi ya Hull City ambapo amepokea taarifa kwamba Terry hatoweza kucheza katika mchezo huo.

Chelsea ambayo kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ulinzi ikiwa kati ya orodha ya timu zilizoruhusu mabao mengi kwa sasa katika ligi kuu ya Uingereza kwa sasa inakabiliwa na kuhaha kuweza kutengeneza ukuta imara.

John Terry ambaye pia ni nahodha mkuu wa timu hiyo alipata majeruhi katika game iliyoisha kwa sare ya bao 2-2 dhidi ya Swansea aliumia na ikatazamiwa atakaa nje kwa muda kidogo, lakini baada ya uchunguzi wa daktari ikagundulika hajaumia sana kwa maana hiyo atawai kurudi dimbani.

Ambapo mpaka katikati ya wiki hii ikategemewa kwamba atawai kurudi kwenye game ya jumamosi hii dhidi ya mapaka, Hull city. Na majibu yaliyokuja ni kwamba katika game hiyo Terry hatokuwepo kutokana hajapona vizuri na badala yake inategemewa na hata kuaminika atarudi game dhidi ya Leicester city wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.