Showing posts with label Gallery. Show all posts
Showing posts with label Gallery. Show all posts

Sunday, 14 May 2017

Mtoto wa nyoka ni wa nyoka tu

Baada ya juzi kaka zao kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Uingereza na watoto na wao wameendeleza moto uleule.

Chelsea U18s ambayo ni timu ya vijana ya wa umri chini ya miaka 18 na wao wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya taifa kwa timu za umri wao. Chelsea U18s imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa historia na ukubwa wa hali ya juu mara baada ya kupata ubingwa huo wakiwa wamefanikiwa kufunga magoli 115 toka mwaka 2015 na kupata 'cleansheets' 18 kwa msimu huu. Lakini pia wametwaa na kombe la taifa, kwa mafanikio hayo wamevunja rekodi baada ya kupata mafanikio makubwa zaidi toka kufanya hivyo mwaka 1961.

Hongereni vijana, mnaipa hadhi chama la Chelsea....

Saturday, 13 May 2017

Chelsea bingwa Premier League 2016-2017

Toka Roman Abramovich ainunue Chelsea, hizi ndizo timu zilizobeba makombe ya Ligi kuu Uingereza
Chelsea 🏆×5
Man utd 🏆×5
Man city 🏆×2
Arsenal 🏆×1
Leicester 🏆×1

Chelsea bingwa wa EPL 2016-2017

Friday, 12 May 2017

Bado masaa machache Chelsea kutangazwa rasmi

Je wajua kama usiku wa leo Chelsea akitangazwa kuwa bingwa basi kila mchezaji atapata bonasi ya £217,000.

PL; Kuelekea West Bromwich vs Chelsea tarehe 12-May

Takwimu na rekodi za timu hizo

Pedro na tunzo ya goli bora la mwezi

Pedro Rodriguez ameshinda tunzo ya goli bora la mwezi Aprili alilofunga dhidi ya Everton katika ushindi wa 3-0

Hongera Pedro

Wednesday, 10 May 2017

Chelsea na utamu wake

Wachezaji wa Chelsea wenye mabao zaidi ya 10 katika ligi tofauti msimu huu...

>Diego Costa katika ligi kuu Uingereza au Epl ana magoli 20
>Tammy Abraham katika ligi daraja la kwanza la Uingereza au Championship akiwa kwa mkopo ana magoli 22
>Betrand Traore katika ligi kuu ya Uholanzi akiichezea Ajax kwa mkopo ana magoli 12

Friday, 14 April 2017

Chelsea na utamu wake

Ujue sio kawaida japo wengi wanachukulia kawaida na hawalitazami kiundani...

Kumbe yule nyota wa Monaco ya Ufaransa, Kylian Mbappe naye ni shabiki nguli wa Chelsea. Nashangaa timu kama Chelsea kupendwa namna hii ni kwa sababu gani nakosa majibu.

Na hapo hapo yule kocha wa Sevilla ambaye kabla alikuwa anaifundisha Chile, Jorge Sampaoli alisikika akisema aliamua kuachana na Chile akitaka kutua Chelsea ndipo Roman Abramovich akampata Conte.

Lukaku naye kamwambia kocha wake wa Everton, Koeman kwamba hatosaini mkataba mpya na timu hiyo na Didier Drogba alisema ameongea na Lukaku na inaonekana kwa asilimia kubwa anataka kuja Chelsea

Sanchez naye kaifananisha Arsenal na nguo isiyomfaa tena na anataka kutua Chelsea

Kumbuka uhamisho wa Mikel ilikuwa atue Man utd lakini akaja Chelsea, bila kusahau uhamisho wa Willian naye alishafanyiwa vipimo na Tottenham na akaikacha na kutua Chelsea.

Eto'o aliachana na mshahara mnono wa Anzhi na kutua Chelsea. Matic alienda Benfica kama kwa udhalilishaji flani lakini bado akarudi palepale, usimsahau pia Luiz alivyoondoka kwa majungu lakini now anavaa jezi namba 30 ya Chelsea.

Bado naamini Yuda Iskarioti alienda Man6 ili kuwapoteza kabisaaaa kwenye ulimwengu wa soka, ni wakala wetu aliyekuwa kwenye kambi ya adui...
#AtarudiKustaafiaDarajani

Alex goal vs Liverpool

Tarehe kama ya leo 14-April-2009
Mlinzi wa kati wa Chelsea, Alex alifunga goli la mpira wa adhabu katika mchezo dhidi ya Liverpool katika kombe la klabu bingwa ya Ulaya maarufu kama Uefa Champions, na mpira uliisha kwa sare ya 4-4 na Chelsea kufuzu kwa jumla ya magoli 7-5.

Chukua hiyo ya Fabregas

Je wajua?
Katika maisha yake ya soka ndani ya Chelsea, Cesc Fabregas ni mechi moja aliyofunga goli na mechi kuisha Chelsea ikapoteza mchezo. Mchezo wa Chelsea dhidi ya Crystal Palace ndio mchezo pekee kwa Fabregas kufunga alafu Chelsea ikapoteza kwa kufungwa 2-1.

Photos; Hii ndio mishahara ya Chelsea

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.