Friday, 14 April 2017

Chelsea na utamu wake

Ujue sio kawaida japo wengi wanachukulia kawaida na hawalitazami kiundani...

Kumbe yule nyota wa Monaco ya Ufaransa, Kylian Mbappe naye ni shabiki nguli wa Chelsea. Nashangaa timu kama Chelsea kupendwa namna hii ni kwa sababu gani nakosa majibu.

Na hapo hapo yule kocha wa Sevilla ambaye kabla alikuwa anaifundisha Chile, Jorge Sampaoli alisikika akisema aliamua kuachana na Chile akitaka kutua Chelsea ndipo Roman Abramovich akampata Conte.

Lukaku naye kamwambia kocha wake wa Everton, Koeman kwamba hatosaini mkataba mpya na timu hiyo na Didier Drogba alisema ameongea na Lukaku na inaonekana kwa asilimia kubwa anataka kuja Chelsea

Sanchez naye kaifananisha Arsenal na nguo isiyomfaa tena na anataka kutua Chelsea

Kumbuka uhamisho wa Mikel ilikuwa atue Man utd lakini akaja Chelsea, bila kusahau uhamisho wa Willian naye alishafanyiwa vipimo na Tottenham na akaikacha na kutua Chelsea.

Eto'o aliachana na mshahara mnono wa Anzhi na kutua Chelsea. Matic alienda Benfica kama kwa udhalilishaji flani lakini bado akarudi palepale, usimsahau pia Luiz alivyoondoka kwa majungu lakini now anavaa jezi namba 30 ya Chelsea.

Bado naamini Yuda Iskarioti alienda Man6 ili kuwapoteza kabisaaaa kwenye ulimwengu wa soka, ni wakala wetu aliyekuwa kwenye kambi ya adui...
#AtarudiKustaafiaDarajani

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.