Showing posts with label Chelsea B. Show all posts
Showing posts with label Chelsea B. Show all posts

Tuesday, 1 August 2017

Mambo 4 unayopaswa kuyajua kwa kinda mpya Gilmour

Chelsea inaripotiwa kushinda vita juu ya kumsajili kinda anayetajwa kuwa na uwezo mkubwa, Billy Gilmour anayeichezea kwa sasa Rangers ya Scotland.

Chelsea inaripotiwa kutoa kiasi cha paundi 500,000 ili kumnasa kinda huyo mwenye miaka 15.

Na haya ndo mambo manne unayopaswa kuyajua juu ya mchezaji huyo.

1. Alibakiza kidogo kuweka rekodi ya kinda zaidi
Derek Ferguson ndiye anashikilia rekodi ya mchezaji kinda zaidi kucheza katika mechi ya kiushindani klabuni Rangers aliweka rekodi hiyo akiwa na miaka 16 na siku 24. Lakini kwa Billy Gilmour alibakiza kidgo kuivunja rekodi hiyo mara baada ya kuwa kati ya wachezaji wa akiba katika kikosi cha Rangers mapema mwaka huu ambapo alitimiza miaka 16 mwezi Juni tarehe 11. Kama angecheza kwenye mchezo huo aliokuwa mchezaji wa akiba basi angeweka rekodi hiyo ya kuwa kinda zaidi.

2. Rangers wameangaika kumzuia
Klabu inayomkuza mchezaji huyo ya nchini Scotland, Rangers imeshajalibu sana kumshawishi kinda huyo ili kuendelea kubaki. Lakini ilishawai kufika kwa wazazi wa mchezaji huyo ambapo kocha wa Rangers alifika na kuwashawishi wazazi waweze kumbakisha, ila wazazi waling'ang'ania kwamba mtoto wao ni lazima akacheze Chelsea.

3. Ana mafanikio makubwa kwenye soka
Akiwa timu ya taifa anayoichezea ya Scotland U-16 akiwa sambamba na kinda mwengine anayefukuziwa na Chelsea, Karamoko Dembele yule anayeichezea Celtic ilimenyana na Jamhuri ya Ireland U-16 katika mashindano ya vijana aliiwezesha timu yake kumaliza kama mshindi wa pili.

Lakini Billy Gilmour alisifika kwa uwezo wake wa hali ya juu katika unyumbulikaji wake na uwezo wa kutoa pasi.

4. Anaendana sana na mfumo wa Chelsea
Akademi ya Chelsea imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi hiki cha karibuni ikiwa imekuza vipaji vingi ambao mifano ya vipaji hivyo ni Charly Musonda, Nathaniel Chalobah na Ruben Loftus Cheek na kwa jinsi anavyocheza Billy Gilmour anaendana sana kimfumo na akademi ya Chelsea.

Sunday, 14 May 2017

Mtoto wa nyoka ni wa nyoka tu

Baada ya juzi kaka zao kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Uingereza na watoto na wao wameendeleza moto uleule.

Chelsea U18s ambayo ni timu ya vijana ya wa umri chini ya miaka 18 na wao wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya taifa kwa timu za umri wao. Chelsea U18s imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa historia na ukubwa wa hali ya juu mara baada ya kupata ubingwa huo wakiwa wamefanikiwa kufunga magoli 115 toka mwaka 2015 na kupata 'cleansheets' 18 kwa msimu huu. Lakini pia wametwaa na kombe la taifa, kwa mafanikio hayo wamevunja rekodi baada ya kupata mafanikio makubwa zaidi toka kufanya hivyo mwaka 1961.

Hongereni vijana, mnaipa hadhi chama la Chelsea....

Monday, 6 March 2017

Video; Lucas Piazon

Unamkumbuka yule dogo anaitwa Lucas Piazon mwenye uraia wa Brazil ambaye kwa sasa anaichezea Fulham kwa mkopo? Basi ndo huyu hapa nimekuwekea video yake uuone utamu wake.

Wednesday, 22 February 2017

Abraham kurudi darajani

Kinda wa Chelsea aliyekuwa kwa mkopo katika timu ya Bristol city, Tammy Abraham anatarajiwa kurudi Chelsea ili kuweza kufanyiwa matibabu baada ya kupata majeruhi.

Saturday, 18 February 2017

FA Youth Cup; Chelsea vs Newcastle au Tottenham

Timu ya vijana wa umri chini ya miaka 18 ya Chelsea watamenyana na mshindi kati ya Newcastle U18 watakaocheza na Tottenham U18 katika kombe la FA kwa vijana (FA Youth Cup)

Mchezo wa robo fainali Chelsea U18 ilifuzu baada ya kuifunga Leicester U18 katika dimba la King Power kwa goli 1-0.

Na kwa maana hiyo mshindi baina ya Newcastle U18 na Tottenham U18 itasababisha pia kujua kama Chelsea U18 katika nusu fainali watacheza nyumbani au ugenini.

Endapo Tottenham U18 akamfunga Newcastle U18 basi nusu fainali dhidi ya Chelsea U18 itachezewa White Hart Lane dimba la Tottenham kwa maana hiyo Chelsea U18 watafululiza michezo miwili wakiwa ugenini.

Au kama Newcastle U18 wakishinda na kufuzu basi Chelsea U18 watacheza nyumbani nusu fainali hiyo.

Na kwa wale wasiojua Chelsea U18 anacheza pia mdogo wa Nathan Chalobah anayeitwa Trevoh Chalobah lakini wakati kaka yake akicheza kikosi cha wakubwa akicheza kama kiungo basi mdogo wake huyu anacheza kama mlinzi wa kati na mara nyingi amekuwa akiwa karibu na John Terry.

Nitaendelea kukujuza yote kuhusu habari za timu hii ya Chelsea U18 katika kombe hili.

Thursday, 16 February 2017

Musonda Jr. awapa kitisho akina Willian

Kinda anayetajwa kuwa na kipaji cha hali ya juu alielelewa kwa muda mrefu ndani ya Chelsea academy akitokea timu ya vijana ya Anderlecht iliyopo Ubelgiji, Charly Musonda au mwenyewe anajiita Musonda Jr. ambaye ni mchezaji halali wa Chelsea ingawa kwa sasa anakipiga Real Betis ya Hispania ametoa tahadhari kwa akina Willian na Pedro.

Charly Musonda ambaye pia yupo karibu na mdogo wa Eden Hazard aitwaye Thorgan Hazard amekuwa akimwambia sana Thorgan kwamba msimu ujao anarudi Chelsea lakini kurudi kwake anarudi kuja kufanya kazi na kwa maana hiyo wale wanaocheza nafasi moja na anayocheza yeye wajiandae.

Musonda Jr. aliezaliwa mwaka 1996 mwezi wa 10 ameonekana kuwa mwendelezo wa kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji, ambapo chenga zake na uwezo wake uwanjani umekuwa ukiwatoa denda mascout wa timu mbalimbali ingawa yeye amekuwa akisisitiza kwamba bado anataka kurudi Chelsea.

Chelsea watoto kama wakubwa

Timu ya Chelsea ya umri chini ya miaka 18 imefanikiwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Leicester ya chini ya miaka 18 katika dimba la ugenini. Goli hilo lilifungwa na Ike Ugbo.

Monday, 13 February 2017

Tammy Abraham afanya makubwa

Kocha wa timu ya Bristol city inayoshiriki ligi ya Championship, Lee Johnson amemsifu kinda wa Chelsea anayecheza kwa mkopo katika timu yake, Tammy Abraham ambaye mara nyingi anacheza kama mshambuliaji au kiungo mshambuliaji.

Kocha huyo amemsifu sana kinda huyo na hakuacha kuwapongeza Chelsea na kuwashuruku kwa kumpatia mchezaji huyo akacheze kwa mkopo katika timu hiyo akisema mpaka Chelsea wamekubali kumpatia mchezaji huyo basi wana imani kubwa na timu hiyo ya Bristol city. Tammy Abraham ana umri wa miaka 19 akiwa amezaliwa mwezi Oktoba mwaka 1997.

Friday, 10 February 2017

Robo fainali ya FA

Hatimae vijana wa Chelsea ya vijana (Chelsea B) itamenyana na Leicester ya vijana (Leicester B) katika robo fainali ya kombe la vijana la FA siku ya tarehe 15-February-2017 mishale ya saa 22:15 usiku.

Christian Atsu

Mmoja kati ya wachezaji ambao nategemea makubwa kutoka kwake. Anaitwa Christian Atsu Twasam akiwa na miaka 25 ambaye kiasili ni mtu wa Ghana. Sisi kama mashabiki wa Chelsea tunategemea makubwa kutoka kwake ingawa kwa sasa yupo kwa mkopo katika timu ya Newcastle united inayoshiriki ligi ya Championship ya Uingereza.

Amekuwa anafanya makubwa kwa timu zote ambazo amekuwa akicheza kama FC Porto, Everton na Newcastle kwa sasa.

Alisajiliwa na Chelsea mwaka 2013 akitokea FC Porto ambapo dau lake lilikuwa £ 3.5 milioni (paundi milioni 3.5) na akapelekwa kwa mkopo moja kwa moja nchini Uholanzi.

Style yake ya uchezaji haikosani sana na ya Victor Mosses ambaye naye alitua Chelsea akitokea Wigan Athletic na baada ya kutua Chelsea aliangaika sana kupata nafasi ya kucheza huku akipelekwa timu mbalimbali kwa mkopo kama Liverpool. Lakini kwa sasa amekuwa mchezaji tegemeo kwa Chelsea na hata timu yake ya taifa ya Nigeria.

Kwa maana hiyo basi Christian Atsu nae inabidi akaze buti ili kufikia mafanikio na baadae akaja kuwa bora.

Monday, 26 September 2016

Tammy Abraham ang'aa

Kinda wetu aliyeibukia katika academy au shule ya vipaji Tammy Abraham ambae yupo kwa mkopo katika timu ya Bristol city inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) jumamosi aling'aa dhidi ya Fulham katika ushindi wa goli 4-0 ugenini.

Johnny terrry a.k.a Bila yeye tunafungwa

kapteni wa chelsea first team

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.