Monday, 24 April 2017

Antonio Conte: Ni heri nifungwe kuliko...

Nyota wa Chelsea, Cesc Fabregas ametoa neno kuhusu kiwango na ujuzi wa mchezaji mwenzake, Eden Hazard mara baada ya mchezo wa kombe la FA ulioipa ushindi Chelsea na kufanikiwa kufika fainali kwa magoli 4-2.

"Mara nyingi nimekuwa namwambia Hazard ye ni mchezaji bora sana duniani, anazidiwa na mchezaji mmoja tu. Messi. Na njia pekee ili aweze kushindana na kuwa bora zaidi basi awe mchoyo." alisema Fabregas
"Unakuta muda mwengine tunashambulia ghafla na tunabaki wachezaji wawili dhidi ya wawili wa timu pinzani lakini Hazard atakupa mpira ili ushinde. Huwa namwambia una uwezo wa kwenda mwenyewe na kufunga kwanini unatoa pasi?" aliongezea Fabregas akimshawishi Hazard ili awe anafunga zaidi ya ili kuziilisha jinsi gani alivyobora

Lakini alipoulizwa Antonio Conte kuhusu kauli hiyo ya Fabregas kama anakubaliana nayo alijibu
"Hapana. Tena hapana. Sijawai kuamini kama mchezaji bora ni lazima awe mchoyo ila anahitaji acheze na timu ili aonyeshe ubora wake" alisema Antonio Conte.
"Nashangazwa na fikra kama hizo za Fabregas lakini mi sikubaliani nazo kabisa. Ni heri nipoteze mchezo kuliko kuwa na mchezaji mmoja mchoyo asiyetaka kucheza kama timu."

Antonio Conte ataiongoza tena Chelsea siku ya Jumanne ya tarehe 27-April katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Southampton katika uwanja wa Chelsea muda ukiwa saa 22:00

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.