Thursday, 3 August 2017

Wenger amtumia ujumbe Sanchez

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemtumia ujumbe mshambuliaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez ambaye ni raia wa Chile.

Sanchez amepokea ujumbe kutoka kwa kocha huyo akimwambia kama akimuuza na kuondoka klabuni hapo basi asitegemee kuuzwa kwenda Chelsea ama Manchester city klabu zinazotajwa kumuwania.

Alexis Sanchez ambaye amebakisha mwaka mmoja klabuni hapo amekuwa akihusishwa na klabu hizo mbili lakini kocha Wenger ataki kurudia makosa aliyoyafanya kwa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Robin Van Persie ambapo aliuzwa kwenda Man utd lakini badala yake akawa moto na kuifunga klabu yake ya zamani. Kwa maana nyengine Wenger hataki kuwauzia maadui zake silaha.

Na kwa maana hiyo inaonekana safari yake ya kujiunga na Bayern Munich klabu ambayo nayo imemfukuzia kwa muda.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.