Thursday, 3 August 2017

Wenger aikandia Chelsea

Kocha wa Arsenal, Arsenal ameikandia Chelsea juu ya usajili ulioifanya klabu hiyo iliyo chini ya kocha muitaliano, Antonio Conte.

Arsene Wenger amesema "kwa upande wa Bakayoko kuchukua nafasi ya Matic ni sawa maana hata Bakayoko ana nguvu pia. Lakini kwa upande wa Morata kuchukua nafasi ya Diego Costa sizani kama ni chaguo sahihi" alisema kocha huyo ambaye anaenda kuiongoza klabu yake kumenyana na Chelsea katika mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Chelsea siku ya jumapili tarehe 06-Agosti.

Morata amesajiliwa akitokea Real Madrid kwa dau lililomfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kikosini na pia kuwa mhispania ghali kwa dau la paundi milioni 70.

Arsenal imekutana na Chelsea mara nne kwa kipindi ambacho Chelsea inaongozwa na Antonio Conte ambapo imekutana mara 2 katika michezo ya ligi ambapo huko Chelsea ilishinda mmoja kwa mabao 3-1 na Arsenal katika uwanja wa Fly Emirates ilishinda 3-0 katika mzunguko wa kwanza wa ligi. Lakini zikamenyana tena kwenye fainali ya kombe la FA na Arsenal akashinda kwa 2-1 kabla ya mchezo wa kirafiki uliochezwa China na Chelsea ikashinda kwa mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.