Mwanasheria Ricardo Cardoso ambaye ni mwanasheria wa nyota wa Chelsea, Diego Costa aishutumu Chelsea juu ya usajili wa mteja wake, Diego Costa.
Mwanasheria huyo ameishutumu Chelsea akidai haitendi haki juu ya mchezaji huyo na kwamba inaweka ngumu katika mauzo ya mchezaji huyo anayedai anataka kuondoka na klabu anayoitaka ni Atletico Madrid.
Chelsea inashutumiwa na mwanasheria huyo kwamba inaweka vikwazo vingi juu ya mchezaji huyo ili asiondoke na amepanga kuishtaki timu ya Chelsea akidai haimtendei haki mteja wake.
Diego Costa alitumiwa ujumbe mfupi na kocha wa Chelsea, Antonio Conte akiambiwa haihitajiki katika mipango ya kocha huyo na pia kocha huyo aliwai kuhojiwa kuhusu ishu ya mchezaji huyo lakini akasema ishu yake yeye na Costa alishaimaliza na Costa mwenyewe anaelewa kwamba hatokuwa na nafasi katika mipango yake kwa maana hiyo kilichobaki ni yeye kuongea na wakala wake ili amtafutie klabu ya kucheza msimu ujao.
Costa mwenyewe anataka kuamia Atletico Madrid lakini klabu hiyo imefungiwa kufanya usajili wowote hali inayomfanya Costa kupata ugumu kutimiza lengo lake la kuungana na kocha Diego Simeone.
Mwanasheria wa mchezaji huyo alihojiwa na chombo kimoja akasema mchezaji huyo ni wa kucheza klabu moja tu, nayo ni Atletico Madrid na sio nyengine. Sasa je Costa ataenda vipi Atletico Madrid wakati imefungiwa? Ndio swali ambalo mwanasheria huyo amewaachia watu!
Tusubiri tuone itakuwaje!
No comments:
Post a Comment