Victor Moses, mchezaji wa Chelsea aliyesafiri mpaka Uingereza kama mkimbizi baada ya machafuko nchini kwao Nigeria ana habari tamu na habari chungu.
Ngoja nianze na habari tamu;
Habari tamu ni kwamba Victor Moses atacheza katika mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Arsenal siku ya jumapili tarehe 06-Agosti, tofauti na habari zilizotoka mwanzo kwamba atatumikia adhabu.
Lakini kwa habari chungu;
Kutokana na ile kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo dhidi ya Arsenal katika mchezo wa fainali ya kombe la FA ambapo mwanzo ilidhaniwa kwa kadi ile basi ingemgharimu kuukosa mchezo wa Ngao ya Hisani, lakini imebainika kumbe ataukosa mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Burnley utakaochezwa jumamosi ijayo tarehe 12-Agosti.
No comments:
Post a Comment