Thursday, 3 August 2017

PL; Siku 8 zimebaki

Siku 8 zimebaki kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Uingereza maarufu kama Premier League msimu wa 2017-2018.

Leo tunawaangalia wachezaji waliouzwa na Chelsea kujiunga na timu nyengine mpaka sasa;

John Terry, baada ya kucheza kwa mafanikio katika klabu yake ya nyumbani jijini London alipozaliwa, ameichezea Chelsea kwa miaka 22 kwa mafanikio makubwa, miaka 14 akiwa kama nahodha kwa mataji kibao akiwa nahodha wa kwanza wa Uingereza kutwaa mataji 5 ya ligi. Ameondoka Chelsea kama mchezaji huru mara baada ya kumaliza mkataba wake ambapo kwa aina ya sheria ya Chelsea mchezaji mwenye mwaka 1. Mkongwe huyu alisema hataki kuamia klabu iliyopo ligi kuu ili asicheze dhidi ya Chelsea. Amejiunga na Aston Villa.

Nemanja Matic, alikuwa ndiye kiungo aliyezuia mpira mara nyingi msimu wa 2014-2015 kuliko kiungo yeyote, msimu ambao Chelsea ilimaliza kama bingwa wa Premier League. Ameuzwa kwenda Manchester utd kwa dau la paundi milioni 40 ambapo huko ameungana na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.

Nathaniel Chalobah, huyu ni mchezaji kinda wa Chelsea raia wa Uingereza akiwa alijiunga na akademi ya Chelsea akiwa na miaka 10 tu. Hajaichezea Chelsea michezo mingi ingawa katika mchezo wa kwanza kuichezea Chelsea ilikuwa kaingia kama mchezaji wa akiba na akatoa pasi murua ya goli lililofungwa na kinda mwenzake Betrand Traore. Amejiunga na Watford kwa uhamisho usiokuwa na kipengele cha kurudi tena Chelsea, amejiunga kwa mkataba wa miaka 5.

Betrand Traore, kinda huyu nae aliichezea Chelsea michezo michache kabla ya kupelekwa Ajax kwa mkopo ambako huko alicheza kwa mafanikio mpaka kuisaidia klabu hiyo kufika fainali ya kombe la Ueropa ambapo walifungwa na Man utd. Huyu amejiunga na Olympique Lyon ya Ufaransa.

Dominic Solanke, baada ya kuisaidia timu ya taifa ya Uingereza akichaguliwa akitokea kwenye akademi muda ambao alikuwa ameshasajiliwa na Liverpool. Aliisaidia Uingereza ya vijana kutwaa kombe la dunia kwa ngazi ya vijana na yeye kuibuka kuwa mchezaji bora wa mashindano.

Nathan Ake, huyu naye amejiunga na AFC Bournemouth ya Uingereza, klabu ambayo nusu msimu uliopita aliichezea klabu hiyo kwa mafanikio makubwa japo kwa mkopo. Lakini aliichezea klabu hiyo kabla ya kurudishwa na Conte kurudi Chelsea ili kupigania kutwaa taji wakati ambao Chelsea ilikuwa kwenye jitihada za kutwaa taji hilo. Lakini sasa amerudishwa klabuni hapo kwa kuuzwa kabisa.

Asmir Begovic, baada ya kusajiliwa akitokea Stoke city na Jose Mourinho alicheza kwa mafanikio chini ya makocha wote watatu katika misimu minne ambao ni Jose Mourinho, Guus Hiddink na Antonio Conte ambapo chini ya makocha hao ameisaidia Chelsea kutwaa mataji mawili ya ligi kuu na taji moja la ligi.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.