Wednesday, 2 August 2017

Swali jengine gumu kwa Diego Costa

Hapa sasa Costa anatakiwa atulize kichwa kufanya maamuzi ili yasimuharibie na akashuhudia akiachwa kwenye safari ya timu yake ya taifa ya Hispania ikisafiri na kwenda zake kombe la dunia 2018 nchini Urusi huku ye akibaki asijue cha kufanya.

Ujue imekuwaje?
Klabu ya AC Milan imerudi tena kwa mchezaji huyo na kuweka dau tena ili kumnunua mshambuliaji huyo ambaye anaonekana kutokuwa na nafasi tena klabuni Chelsea huku akiambiwa na Antonio Conte hana mipango naye, na ikumbukwe wa kuchukua namba yake ashapatikana. Alvaro Morata.

Chelsea inataka dau la paundi milioni 55 ili kumwachia mchezaji huyo ambaye binafsi anataka kuungana na klabu yake ya zamani, Atletico Madrid.

Lakini Atletico Madrid wana kifungo cha kutofanya usajili wowote mpaka mwezi januari.

Sasa je Diego Costa achague kwenda AC Milan ili ajihakikishie kucheza kombe la dunia nchini Urusi, au aendelee na nia yake ya kurudi Atletico Madrid na nafasi yake ya kucheza kombe la dunia ibaki kuwa historia?

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.