Wednesday, 2 August 2017

Chelsea yaweza kumtwaa Drinkwater kirahisi

Kiungo Danny Drinkwater wa Leicester city anatazamwa kuweza kutua Chelsea muda wowote kuanzia sasa.

Mapema wiki hii Chelsea ilishuhudia kiungo wake Nemanja Matic akijiunga na mahasimu Man utd na kwa hivyo kuna nafasi ya kiungo inahitajika ili kuziba pengo la mserbia huyo, na Drinkwater anaonekana ndo chaguo la kocha Antonio Conte.

Wachambuzi wengi wa soka wanaamini itakuwa ngumu kwa Drinkwater kukataa ofa kama hiyo ukizingatia anatakiwa na klabu mabingwa wa taji la ligi kuu Uingereza.

Lakini pia huenda N'golo Kante akatumika katika kukamilisha usajili huu kwa maana walishawai kucheza timu moja na wakacheza kwa mafanikio makubwa.

Kama hiyo haitoshi inaonekana kama Drinkwater anataka kuitwa na kocha wa England kwenda kucheza kombe la dunia mwaka kesho nchini Urusi basi itamlazimu kwenda Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.