Chelsea ambayo inaangaika sokoni kutafuta wachezaji watakaokiimarisha kikosi hicho kabla ya kuuanza msimu mpya ambapo jioni ya leo itashuka uwanjani kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Burnley. Jioni ya saa 17:00.
Katika kuangaika kwake kusaka wachezaji hao, iliripotiwa imekuwa ikipendezwa na mlinzi wa Valencia, klabu ya nchini Hispania, Joao Cancelo aliyesajiliwa na timu hiyo akiwa kama mchezaji wa mkopo kabla ya uhamisho kukamilishwa na kinda huyo kuwa mchezaji rasmi wa Valencia akitokea Benfica.
Lakini pamoja na Chelsea kutajwa juu ya mchezaji huyo, kiongozi wa klabu hiyo ya Valencia ameibuka na kusema hajui lolote kuhusu Chelsea kumtaka nyota huyo mwenye uraia wa Ureno. Ambapo hii inamaanisha Chelsea haijapeleka ofa yoyote kwa mchezaji huyo ambaye Conte anamtaka ili kuja kupambana na Victor Moses katika nafasi ya winga mkabaji au right wing-back.
Kinda huyo mwenye miaka 21 ametajwa na Antonio Conte ambaye inaelezwa walishatumwa maskauti wa Chelsea mara mbili kwenda kumtazama nyota huyo.
No comments:
Post a Comment