Mchezaji nyota wa Everton raia wa Uingereza, Ross Barkley bado hajaonekana ataichezea timu gani msimu ujao.
Nyota huyo ambaye kocha wake wa Everton, Ronald Koeman alishakiri kwamba mchezaji huyo hatoendelea kuwa klabuni mwake alikuwa anatajwa kwa karibu kutakiwa na Chelsea ingawa Koeman anasema hakuna ofa yoyote iliyopelekwa kwa mchezaji huyo.
"mpaka sasa hakuna ofa iliyoletwa kwa Barkley, na anafanya mazoezi na timu (Everton) na kama ikiendelea hivyo basi msimu ujao anaweza kuendelea kuwepo hapa" alisema kocha Koeman juu ya nyota huyo.
Chelsea ilitajwa kuwataka nyota watatu wa kiingereza ambao ni Oxlade Chamberlain wa Arsenal, Ross Barkley na Danny Drinkwater wa Leicester ingawa mpaka sasa inaelezwa ni ofa ya Chamberlain pekee ndiyo ambayo imepelekwa kumtaka nyota huyo.
No comments:
Post a Comment