Antonio Conte wa Chelsea bado anaisaka saini ya mlinzi wa kushoto raia wa Brazil, Alex Sandro.
Sandro amekuwa akifukuziwa kwa karibu na Antonio Conte ambaye mpaka sasa ashatumia kiasi cha paundi milioni 130 katika usajili. Na sasa anatazamia kumsajili mlinzi huyo akiwa kwenye jitihada za kuijenga timu kuelekea msimu mpya utakaokuwa na mechi nyingi kwa Chelsea.
Chelsea ilitajwa kutia dau la euro milioni 60 ambazo ni sawa na paundi milioni 54 lakini matajiri wa Turin, Juventus waligoma kupokea dili hilo. Lakini sasa inaelezwa Chelsea imepeleka dau jengine mezani kwa Juventus ili kumsajili mchezaji huyo. Imepeleka ofa ya euro milioni 68 ambazo ni sawa na paundi milioni 60.
No comments:
Post a Comment