Antonio Conte bado hajaridhika. Hajaridhika kwa sajili alizozifanya baada ya kuwanasa Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko, Willy Caballero na Alvaro Morata ambapo kwa sajili hizo mpaka sasa ashatumia paundi milioni 130.
Lakini kocha huyo hajaridhika, na sasa anataka saini za anawafukuzia nyota watatu raia wa Uingereza.
Ross Barkley, nyota huyu wa Everton anatakiwa kwa karibu na Chelsea ambapo nyota huyo anatakiwa pia na Tottenham ingawa kwa Tottenham inaonekana kushindwa mbio hizo mara baada ya Everton kumpa ofa mchezaji huyo ili kuongeza mkataba na klabu hiyo ambapo amepewa ofa ya mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki. Kiasi ambacho kinaonekana ni kizito kwa Tottenham kuipiku mshahara huo.
Oxlade Chamberlain. Nyota huyo wa Arsenal amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Arsenal, na Chelsea inatazamiwa kuweka dau la paundi milioni 25 ili kumsajili nyota huyo.
Danny Drinkwater, nyota huyu mwenye miaka 27 alifanya vizuri akiwa klabuni kwake Leicester city msimu wa 2015-2016 na kuisaidia klabu yake kutwaa taji la ligi kuu Uingereza kwa mara ya kwanza, lakini msimu uliopita umekuwa mgumu kwake akiwa nje kutokana na majeraha. Chelsea imeanza jitihada za kumsajili nyota huyo ili kuziba pengo la Nemanja Matic aliyetimkia Man utd. Ingawa Leicester hawaonekani kutaka kumuuza mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment