Klabu ya AC Milan bado hawajakata tamaa juu ya uhamisho wa Diego Costa mara baada ya kutaarifiwa uhamisho wa mshambuliaji huyo kujiunga na klabu hiyo haupo.
Diego Costa ambaye ni mshambuliaji wa Chelsea hayupo kwenye mipango ya kocha wa timu hiyo Antonio Conte na sasa inaelezwa kama kuna timu inamtaka basi itoe kiasi cha paundi milioni 55 kiasi ambacho inatajwa AC Milan walikuwa tayari kukitoa.
Lakini mchezaji huyo amegoma kujiunga na klabu hiyo na ikaelezwa uhamisho huo haupo tena lakini sasa klabu hiyo imeamua kurudi tena na sasa inamtaka nyota huyo kwa mkopo.
Diego Costa anataka kuamia klabu ya Atletico Madrid ingawa klabu hiyo imefungiwa kufanya usajili mpaka mwezi januari na kwa hivyo inakuwa haiwezekani kwa nyota huyo kujiunga na timu hiyo aliyotokea.
Lakini pia huenda mchezaji huyo akabaki Chelsea akawa hapo mpaka dirisha dogo la usajili mwezi januari ambapo labda atakuwa na mipango ya kuhamia Atletico kama akitaka mwenyewe.
No comments:
Post a Comment