Saturday, 12 August 2017

PL; Ligi imeanza, Chelsea itacheza dhidi ya Burnley

Ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama Premier League imeanza leo mara baada ya kupita siku takribani 82 kupita toka msimu wa 2016-2017 wa ligi hiyo kuisha, huku Chelsea akiibuka kuwa bingwa.

Siku ya kwanza ambayo ni ijumaa ya tarehe 11-Agosti iliishuhudiwa mchezo wa ligi hiyo kati ya Arsenal dhidi ya Leicester city wakicheza na mchezo huo ukaisha kwa Arsenal kupata ushindi wa jioni wa mabao 4-3. Magoli ya Arsenal yakifungwa na Lacazette, Welbeck, Ramsey na Giroud wakati ya Leicester yakifungwa na Shinji Okazaki na Jamie Vardy aliyefunga mara mbili.

Jioni ya leo kutachezwa mchezo wa bingwa mtetezi yaani Chelsea ambaye kwa sisi Mashabiki wa Chelsea ndio kama bosi wetu atamenyana na Burnley wale watoto wa uwanja mgumu wa Turf Moor.

Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa pale London Magharibi katika mitaa ya Fulham, uwanja wa Stamford Bridge kwenye mishale ya saa 17:00 kwa ukanda wa GMT+3.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.