Wednesday, 9 August 2017

Conte amuelezea Bakayoko

Kocha muitaliano anayeifundisha Chelsea, Antonio Conte amemuelezea nyota mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa akitokea AS Monaco ya Ufaransa, Tiemoue Bakayoko.
"Ni usajili mzuri tulioufanya, na yupo mahari sahihi. Ni mchezaji mwenye nguvu na nilitaka ajifunze mengi haswa juu ya Nemanja Matic katika kuizoea ligi. Lakini hayupo. Kwa maana hiyo kuondoka kwake kunamaanisha tumebakiwa na viungo watatu ambao ni Bakayoko, Cesc na Kante. Hii inamaanisha Bakayoko atatumika sana na sio kutumia muda kujifunza." alisema Conte akimwelezea Bakayoko aliyesajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 40.
Bakayoko mpaka sasa bado hajapona majeraha yake ambapo hii itamaanisha ligi itaanza wakati ye akiwa bado anauguza majeruhi na kwa maana hiyo kwa nafasi ya kiungo itatumika sana na Cesc Fabregas pamoja na Kante.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.