Saturday, 12 August 2017

PL; Chelsea 2 vs 3 Burnley, Chelsea yafungwa na wachezaji 12

Jioni ya leo imekuwa jioni mbaya lwa mashabiki na wapenzi wa soka dunia yote mara baada ya kuishuhudia timu yetu ikipoteza mchezo wake wa kwanza huku kukiwa kuna hujuma nyingi kutoka kwa mwamuzi wa kati wa mchezo huo, Chelsea ikishuhudia wachezaji wake wawili kwa kupewa kadi nyekundu.
Mpira ulianza na kushuhudia Marcos Alonso akipewa kadi ya njano katika dakika ya 3 tu. Baada ya hapo ikafata kwa Gary Cahill nahodha wa Chelsea kupewa kadi nyekundu ambayo haikuwa na mantiki kwa kupewa kadi hiyo ukizingatia haikuwa rafu ya kumzuru au kumuumiza mtu, kadi hiyo ikamfanya Jeremie Boga kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Christensen ili kuimarisha eneo la ulinzi.
Kadi hiyo iliyowaamsha wachezaji wa Burnley na kuanza kulikamia lango la Chelsea, ndipo dakika ya 24, Vokes akaifungia timu hiyo bao la kuongoza.
Wakati mchezo ukiendelea huku wachezaji wa Chelsea wakilalamikia maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi huyo dakika kadhaa tena baadae Cesc Fabregas akaadhibiwa tena kadi ya njano. Bado kama haijaisha Ward akaifungia tena Burnley goli la pili katika dakika ya 39.
Dakika 3 baadae Vokes tena akaifungia Burnley goli la 3 na kuifanya Burnley kuongoza magoli 3-0 mpaka kipindi cha kwanza kinaisha.
Chelsea ilikwenda mapumziko na kurudi ikiwa na hali kubwa na ndo ilikuwa wa kwanza kurudi uwanjani kuwasubiri wachezaji wa Burnley.
Kipindi cha pili kilianza na dakika ya 58 yalifanywa mabadiliko ya pili akaingia Alvaro Morata huku Batshuayi akienda kupumzika.
Mabadiliko hayo yaliipatia Chelsea bao la kwanza lililofungwa na mchezaji ghali wa timu hiyo, Alvaro Morata akipokea pasi tamu kutoka kwa Willian na Morata kufunga kwa kichwa.
Mpira uliendelea kwa kasi kabla ya kumshuhudia tena refa wa kati akimpa tena Cesc Fabregas kadi ya pili ya njano ambayo ilitanguliwa kwa kadi nyekundu.
Lakini mpira ukaendelea na kumshuhudia David Luiz akifunga tena goli la 2 akipokea pasi murua kutoka kwa Alvaro Morata na kufanya matokeo kuwa 3-2.
NB; Nimeandika ripoti hii lakini kiukweli mpenzi msomaji akili yangu haipo sawa, naweza nikawa nimechanganya matukio. Nimekuwekea video ya matukio yote hapa...
Chelsea in Our Hearts Forever

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.