Nyota wa Chelsea, Pedro Rodriguez yupo tayari kuivaa Arsenal katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaomaanisha kufunguliwa rasmi kwa msimu mpya wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2017-2018.
Mchezo huo utachezwa tarehe 06-Agosti ambao utakuwa siku ya jumapili saa 11 jioni kwa ukanda wa mashariki ya Afrika.
Pedro alipata majeruhi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal ambapo katika dakika ya 29 ya mchezo huo aligongwa kichwani na kipa David Ospina na kutolewa nje na kukimbizwa hospitalini. Lakini hakukaa sana hospitalini hapo ikabidi arudishwe Uingereza ambapo huko alikuwa alifanyiwa matibabu zaidi huku akifanya mazoezi mepesi kuwasubiri wenzake.
Lakini pia Victor Moses wa Chelsea ataukosa mchezo huo mara baada katika mchezo wa fainali ya kombe la FA alipata kadi nyekundu na kwa hivyo atatumikia adhabu yake kwa kukosa mchezo huo wa Ngao ya Hisani.


No comments:
Post a Comment