Thursday, 3 August 2017

Huenda akabaki

Huenda Diego Costa akabaki Chelsea. Ndiyo huenda akabaki na kuendelea kuwa mchezaji wa timu hiyo.

Hii imetokea mara baada ya mshambuliaji huyo kukataa ofa ya kujiunga na AC Milan iliyokuwa inamtaka kwa muda, ambapo timu imepanga kurudisha makali yake, mara baada ya kupoteza ubabe wake zaidi ya misimu mitatu sasa. Ambapo mpaka sasa klabu hiyo ya Italia imetumia zaidi ya paundi milioni 150.

Diego Costa ambaye hakuwa na maelewano mazuri na kocha Antonio Conte alitumiwa ujumbe na kocha huyo kwamba hayupo kwenye mipango ya Chelsea na hivyo atafute pa kwenda, na mchezaji alikuwa anatamani kurudi klabu yake aliyotokea Atletico Madrid lakini klabu hiyo ina adhabu ya kutosajili mpaka mwezi januari. Na kama Diego Costa amekataa ofa ya kwenda AC Milan na anaitaka klabu ya Atletico Madrid pekee basi itamlazimu asubiri mpaka Atletico itoke kifungoni ndipo imsajili. Kwa maana hiyo hii inamaanisha ataendelea kubaki Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.