Kiungo mkongwe muingereza aliyeichezea Chelsea, Frank Lampard amesajiliwa tena. Kiungo huyo aliyeweka historia kadhaa ndani ya Chelsea akiwa ndiye mfungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo amesajiliwa.
Mchezaji huyo amesajiliwa na kampuni ya BT Sports ambapo huko atakuwa kama mchambuzi wa michezo haswa mpira wa miguu.
Lampard amesaini mkataba wa kujiunga na kampuni hiyo ambapo kampuni hiyo pia ilishawasainisha wachezaji magwiji kama Rio Ferdinand, na Paul Scholes ambao wao walishaichezea Manchester united.
No comments:
Post a Comment