Katika mchezo wa jumapili wa ngao ya hisani kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal utatumika mtindo mpya wa kupiga matuta imetangazwa na chama cha soka nchini Uingereza maarufu kama FA.
Chama hicho kimetambulisha mtindo huo mpya wa upigaji penalty unaojulikana kama ABBA. Mtindo huo utakuja mara baada ya dakika 90 kuisha kwa matuta na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye kupiga matuta au penalty, ambapo itakuwa badala ya mchezaji mmoja wa timu moja kupiga tuta akimaliza atafata mwengine wa timu nyengine ambapo mtindo huo ndio umezoeleka kutumika ukijulikana kama ABAB yaani AB AB lakini kuanzia katika mchezo huo wa ngao ya hisani utatumika wa ABBA.
ABBA mnapiga kwa wachezaji wawili wa timu moja mnapiga mfululizo, yaani mfano katika fainali hiyo tunafikiria kama ataanza kupiga Pedro wa Chelsea akikosa au akipata anakuja tena mchezaji mwengine wa Chelsea anapiga baada ya hapo wanafata wachezaji wawili wa Arsenal na wao watapiga.
Mtindo huu uliwai kutumika katika michuano ya soka kwa wanawake chini ya miaka 17 kati ya Ujerumani dhidi ya Norway ambapo kama unataka kuuelewa zaidi angalia video yake nimekuwekea hapa chini.
No comments:
Post a Comment