Saturday, 5 August 2017

PL; Siku 6 zimebaki

Siku 6 zimebaki ili msimu mpya wa ligi kuu Uingereza kwenda kuanza ambazo siku hizo ni sawa na kusema ni saa 144 zimebaki.

Lakini wakati muda huo umebaki lakini pia imebaki siku moja kuchezwa mchezo ambao utafungua au utaeleza rasmi kwamba sasa timu zote zipo tayari na zijiandae kwa msimu huo, mchezo ambao unajulikana kama Ngao ya Hisani.

Mchezo huo huchezwa kila pale ligi kuu inapokaribia kuanza ambapo mara nyingi inamhusishwa bingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu uliopita na bingwa wa kombe la FA.

Lakini kama ikitokea bingwa wa ligi kuu akabeba na kombe la FA basi huwa mchezo huo unachezwa baina ya bingwa na mshindi wa pili wa ligi kuu.

Sasa hiyo kesho utakuwa mchezo wa ligi kuu msimu uliopita ambaye ni Chelsea atacheza dhidi ya mshindi wa kombe la FA ambaye ni Arsenal.

Kuelekea katika mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa taifa wa Uingereza unaojulikana kama Wembley mishale ya saa 11 jioni ambapo kuelekea mchezo huo kocha wa Chelsea alisema "tushamaliza michezo ya kirafiki na sasa tunaingia katika mchezo wa kiushindani. Tutacheza kupigania taji" alisema kocha huyo aliyeiongoza Chelsea kutwaa taji lake la tano.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.