Kocha wa Man utd ambaye alishawai kuifundisha Chelsea, Jose Mourinho ameishangaa klabu yake ya zamani kwa kitendo walichokifanya.
Kocha huyo ameishangaa Chelsea juu ya kumruhusu mchezaji Nemanja Matic aungane na kocha huyo kwenye timu yake hiyo ya sasa ya Man utd.
"Baada ya kutua Man utd mwaka jana, niliona kabisa kwamba tunamuhitaji Matic. Na sikuwai kufikiri kwamba Chelsea inaweza kuniuzia mchezaji huyo. Mpaka pale nilipopokea simu ya Matic na akaniambia anataka kuungana na mimi na kuichezea Man utd" alisema kocha huyo anayejulikana kwa kuwa na mbwembwe nyingi.
Kocha huyo aliipatia mataji kadhaa klabu ya Chelsea na aliisaidia kwa asilimia kubwa kuinyanyua na kuwa tishio kwenye ligi kuu ya Uingereza na pia aliisaidia kutwaa mataji ya ligi kuu Uingereza mara mbili mfululizo yaani 2004-2005 na 2005-2006 huku akiweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuiongoza klabu yake kutwaa taji huku ikiwa na uwiano wa magoli mengi ya kufunga, magoli 108 kwa msimu mmoja.
No comments:
Post a Comment