Gwiji wa Chelsea ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa BT Sports, Frank Lampard ameikosoa Chelsea juu ya mtindo wake wa kuuza wachezaji.
Nyota huyo wa zamani wa klabu hiyo amesema leo kupitia chombo kimoja cha habari akisema "ni makosa Chelsea imefanya juu ya kumwachia Nathaniel Chalobah akatimkia Watford" alisema Lampard.
Chalobah ambaye ni zao la akademi ya Chelsea amesajiliwa na Watford ambayo alishaichezea klabu hiyo kwa mkopo na sasa ameuzwa kuichezea klabu hiyo huku Chelsea ikipata tabu baada ya kuwa na viungo wachache ambapo ina viungo watatu ambao ni Tiemoue Bakayoko, Cesc Fabregas na N'golo Kante.
No comments:
Post a Comment