Kuna habari zimefichuka kwamba huenda Chelsea ikajitosa kwenye vita ya kumuwania nyota anayesakwa zaidi kwa sasa na klabu kubwa barani Ulaya, Kylian Mbappe.
Imeelezwa Chelsea imetajwa kuhusishwa na mchezaji huyo pale tu Barcelona watakapokamilisha dili la kumsajili winga machachari wa Chelsea, Eden Hazard.
Eden Hazard anatakiwa na Barcelona akitazamwa kama mrithi na mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya winga mbrazili anayeichezea klabu hiyo ya nchini Hispania, Neymar.
Neymar anatajwa kuhusishwa na mpango wa kujiunga na PSG ya Ufaransa na kama dili hilo likitimia na kwenda sawa basi Barcelona inatazamwa kumsajili Eden Hazard ambaye bosi Roman Abramovich inasemekana yupo tayari kuachana na mbelgiji huyo ili baada ya kumuuza Hazard hiyo pesa atakayolipwa akamsajili Mbappe.
Kylian Mbappe ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye kipaji cha hali ya juu anapendwa sana na tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich kiasi kwamba tajiri huyo anaona ni sawa kumuuza Hazard ili aingie kwenye vita ya kumuwania Mbappe ambaye anatajwa pindi alivyokuwa mtoto alikuwa ni shabiki wa Chelsea.
Sasa je unazani ni sahihi kwa Hazard kuuzwa ili Mbappe anunuliwe?

No comments:
Post a Comment