Danny Drinkwater mwenye miaka 27 amekuwa akitajwa kuwaniwa na Chelsea mara baada ya siku kadhaa klabu hiyo ya jijini London kumpoteza nyota wake Nemanja Matic aliyejiunga Manchester united kwa dau la paundi milioni 40 huku Drinkwater akitajwa kuja kuziba pengo la mserbia huyo.
Mashabiki wengi wakiaminika ni wa Chelsea kupitia mtandao wa Twitter wakisema Chelsea haihitaji mchezaji wa kariba ya Drinkwater huku wengine wakisema kusajiliwa kwa Drinkwater ni kampeni za kumfanya kocha wa Chelsea, Antonio Conte aweze kufanya vibaya msimu unaofata ili atimuliwe.
Lakini pia kuna wengine walihoji kiasi ambacho Chelsea imepokea katika kipindi hiki cha usajili ikitengeneza zaidi ya paundi milioni 150 kwa kuwauza wachezaji kama Juan Cuadrado, Asmir Begovic, Nathan Ake, Nathaniel Chalobah, Dominic Solanke hata Nemanja Matic wangeweza kusajili kiungo aliye na thamani kubwa na mwenye ubora


No comments:
Post a Comment