Mashabiki wa Bayern Munich wamekasirishwa na kiwango duni kilichoonyeshwa na Renato Sanches katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Liverpool uliochezwa jana usiku na kuishuhudia timu hiyo ikiibamiza Bayern Munich mabao 3-0. Huku Renato Sanches kiungo anayewaniwa na Chelsea akilalamikiwa na mashabiki hao kwa kiwango kibovu alichokionyesha katika mchezo.
Mashabiki hao walionyesha hasira zao juu ya mchezaji huyo katika mtandao wa Instagram ambapo walienda kwenye akaunti yake ya mtandao huo na kutuma matusi na hata wengine kumwambia aondoke klabuni hapo, lakini kwa matusi yote aliyoyapata alikuwa anabonyeza kitufe cha kupendezwa na matusi na malalamiko hayo ikitafsiriwa kama kupendezwa kwake na maneno hayo basi anafanya kusudi ili aondoke.
Mchezaji huyo anatajwa kuondoka klabuni hapo ambapo ameichezea kwa muda mfupi baada ya kusajiliwa na klabu hiyo akitokea klabu ya Benfica ya nchini Ureno na sasa mashabiki hawamtaki.
Klabu ya Chelsea inamtaka mchezaji huyu ambaye Bayern Munich hawataki kumuuza ila wanatafuta timu itakayokubali kumchukua kwa mkopo, na Chelsea wao wapo tayari kufanya biashara hiyo.
Klabu nyengine zinazomwania mchezaji huyo ni AC Milan ambao wao wanatajwa wanataka kumsajili kabisa sio kumchukua kwa mkopo na walishapeleka dau la paundi milioni 44 ingawa Bayern Munich waligoma kumuuza, klabu nyengine ni Man utd ambapo inaelezwa Mourinho ni shabiki mkubwa wa mreno mwenzake huyo.
No comments:
Post a Comment