Huenda Chelsea ikafanya usajili mwengine wa haraka na ikaongeza mchezaji mwengine mpya.
Hii inaweza kutokea mara baada ya nyota, winga wa klabu ya Inter Milan, Antonio Candreva kuweza kuachiwa na klabu yake hiyo kuweza kuungana na kocha muitaliano mwenzake, Antonio Conte klabuni Chelsea.
Hii imetokea mara baada ya klabu ya Inter Milan itawawia vigumu kukataa ofa mbili zilizoletwa katika kuwawania mawinga wake wawili, Antonio Candreva akitakiwa na Chelsea na Ivan Perisic akiwaniwa kwa karibu na Man utd.
Lakini Inter Milan imeeleza ipo tayari kumwachia Antonio Candreva aondoke klabuni hapo na sio Ivan Perisic.
Antonio Conte amekuwa akimhitaji kwa karibu mchezaji huyo na huenda hii ikawa taarifa njema kwake na anaweza akalazimisha kwa haraka dili hilo liweze kukamilika kabla ya Inter kubadili mawazo.
No comments:
Post a Comment