Tuesday, 1 August 2017

Cole kurudi Uingereza

Mchezaji gwiji wa zamani wa Chelsea raia wa Uingereza, Ashley Cole ambaye kwa sasa anaichezea timu ya LA Galaxy ya nchini Marekani huenda akarudi nchini kwake kuichezea klabu ya ligi daraja la kwanza nchini humo maarufu kama Championship, klabu ya Birmingham.

Alipoojiwa kuhusu mpango huo alisema "nimebakiza miezi 6 klabuni hapa, kwa hiyo huenda dili hilo likatimia" alisema Ashley Cole ambaye Chelsea walimsajili akitokea Arsenal kwa dau la paundi milioni 5 ukijumlisha na mchezaji William Gallas.

Baada ya kuachana na Chelsea akitengeneza historia kubwa klabuni hapo alijiunga na klabu ya Italia, AS Roma aliyoichezea kwa muda n kujiunga na LA Galaxy anayoichezea mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.