Wednesday, 2 August 2017

Exclusive; Hii ulishaisikia kuhusu Morata

Nadhani hii hujawai kuiskia, sasa leo nakupa kilichojiri kwa mshambuliaji mpya wa Chelsea, Alvaro Morata

Alvaro Morata aliyejiunga na Chelsea katika dirisha hili la usajili akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milioni 70. Kumbe ilikuwa atue Tottenham.

Ndiyo mhispania ilibaki bado kidogo ajiunge na Tottenham iliyo chini na Mauricio Pochettino.

Habari ipo vipi?
Ilikuwa miaka miwili nyuma, ambapo Morata alikuwa bado yupo Real Madrid, ndipo siku moja akapokea simu kutoka kwa kocha wa Tottenham, Pochettino na katika maongezi yao Pochettino alimshawishi mchezaji huyo ajiunge na Tottenham.

Lakini kilichomfanya Morata akatae dili hilo la kujiunga na timu hiyo inayopatikana London Kaskazini sababu kubwa ilikuwa Harry Kane.

Majibu ya Morata kwa Pochettino yalikuwa "unanitaka vipi mimi wakati una Harry Kane"

Yani kumbe isingekuwa Kane kuwepo Tottenham basi leo Morata angevaa jezi za Tottenham inayomilikiwa na tajiri wa kiingereza Joe Lewis.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.