Monday, 7 August 2017

Hazard aomba kuondoka Chelsea

Huenda hii ikawa ni habari mbaya kwa mashabiki wa Chelsea, haswa baada ya kipigo cha jana katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo wengi walitamani winga huyo awepo kwenye kikosi.

Kwa sasa yupo nje akiuguza jeraha alilopata akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Ubelgiji, huyu ni mchezaji bora wa ndani ya klabu ya Chelsea, Eden Hazard.

Hazard inaripotiwa anatamani kujiunga na mabingwa wa Ulaya, Real Madrid ambao wanatajwa kumfukuzia nyota huyo.

Hazard ni chaguo la Zinedine Zidane ambaye ni kocha wa mabingwa hao wa mara 12 wa taji hilo maarufu kama Uefa Champions League ingawa kikwazo cha mapendeleo ya kocha huyo yanakuja baada ya uongozi wa klabu hiyo kumtaka nyota kinda wa AS Monaco, Kylian Mbappe.

Gazeti moja la nchini Uingereza linaeleza kwamba Eden Hazard anaitaka Real Madrid ingawa pia mpinzani wa klabu hiyo, Barcelona nayo inatajwa kumuwania mchezaji huyo ili akachukue nafasi ya Neymar aliyejiunga na PSG.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.