Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema ni kazi ngumu sana kwake kumzuia nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambayea anatajwa kuwaniwa na klabu ya Barcelona.
Barcelpona imemuuza nyota wa klabu yake Neynar Jr. ambaye amejiunga na klabu ya PSG ya Ufaransa kwa dau lililoweka rekodi ya mchezaji ghali zaidi duniani kwa dau la paundi milioni 195 ambapo kwa Barcelona inatajwa kumuwania mchezaji huyo ili kuwa mbadala wa nyota huyo.
Antoni Conte alipoojiwa alisema "Ni kweli hatutopenda kumpoteza mchezaji au wachezaji katika kipindi hiki tukielekea msimu mpya, lakini itakuwa ngumu kwangu kufanya maamuzi juu ya Hazard"
Lakini pia inaelrzwa tajiri na mmiliki wa klabu ya Chelsea, mrusi Roman Abramovich yupo tayari kumuuza Eden Hazard ili dau atakalolipata juu ya mchezaji huyo akitumie kumsajili nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe.
Sasa je mwisho wa siku itakuwaje juu ya hatma ya mbelgiji huyo, Eden Hazard?

No comments:
Post a Comment