Tuesday, 1 August 2017

Fainali ya Ngao ya Hisani yabadilishwa muda

Fainali ya Ngao ya Hisani inayotegemewa kuchezwa tarehe 06-Agosti-2017 kati ya bingwa wa ligi kuu Uingereza yaani Chelsea dhidi ya bingwa wa kombe la FA, Arsenal imebadilishwa muda.

Fainali hiyo mwanzoni ilipangwa kufanyika siku hiyo ila saa 9 mchana kwa muda wa Uingereza ambapo kwa huku katika ukanda wa GMT+3 ingekuwa saa 12 jioni, lakini ili kutaka kupishana na fainali ya kombe la Euro la wanawake wameamua kubadilisha muda na kuirudisha saa moja nyuma, kwa hivyo badala ya kuchezwa saa 12 jioni basi itachezwa saa 11 jioni ambapo kwa Uingereza ni sawa na saa 8 mchana.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.