Saturday, 12 August 2017

Conte atoa neno kuelekea mchezo dhidi ya Burnley

Jioni ya leo kutachezwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uingereza kwa Chelsea itakayocheza dhidi ya Burnley katika uwanja wa Stamford Bridge.

Kuelekea mchezo huo, kocha Antonio Conte amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo ambao walikuwa wana hofu juu ya kiwango kilichoonyeshwa na klabu hiyo katika michezo ya kirafiki iliyocheza klabu huo na katika mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Arsenal.

Katika michezo ya kirafiki, Chelsea imecheza michezo minne ikapoteza miwili dhidi ya Bayern Munich na Inter Milan na kushinda miwili dhidi ya Fulham na Arsenal.

Lakini kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na klabu hiyo wachambuzi wengi wa soka wameitoa klabu hiyo katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini humo. Lakini jioni ya leo katika mkutano na waandishi wa habari kocha huyo amewatoa hofu mashabiki na wapenzi wa timu hiyo mara baada ya kuulizwa kuhusu nafasi ya klabu yake katika kutetea ubingwa wa ligi hiyo.

Kocha Antonio Conte alijibu kwa maneno mafupi akisema "hata msimu uliopita hakuna mtu aliyezani kama tungeutwaa ubingwa" akimaanisha anaweza akaiongoza timu yake pia kuwashangaza watu kama alivyowashangaza msimu uliopita ingawa hakutarajiwa kuipatia klabu hiyo taji hilo.

Na alipoulizwa kama bado anafuraha ya kuendelea ndani ya klabu hiyo alisema hana tatizo klabuni hapo na bado anafuraha kuwa klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.