Klabu ya Southampton imeikata maini Liverpool juu ya mchezaji wake Virgil van Dijk na imeipa kipaumbele Chelsea kuweza kumsajili nyota huyo.
Southampton ilikasirishwa na kitendo kilichofanywa na mawakala wa Liverpool baada ya kufanya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wao Virgil van Dijk bila kuwasiliana na uongozi wa Southampton inayommiliki.
Van Dijk amekuwa akihusishwa pia na kutua Chelsea ambayo imekuwa ikimtaka kwa muda mrefu ili kutengeneza safu imara ya ulinzi kuingia katika michuano ya msimu unaoanza kesho kutwa.
"Hatuwezi kumuuza Van Dijk kujiunga na Liverpool, afadhali tumweke benchi kuliko kuuzwa kwenda kwa timu hiyo, labda kama Chelsea ikionyesha nia na ikifata taratibu tunaweza kuwauzia" ilisema taarifa kutoka uongozi wa Southampton.
Kwa hiyo kikubwa ni kwamba Chelsea ina nafasi kubwa ya kumsajili nyota huyo raia wa Uholanzi mwenye uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati na kiungo mkabaji.
No comments:
Post a Comment