Tuesday, 1 August 2017

Conte amtaka Drinkwater kuziba pengo la Matic

Baada ya Nemanja Matic kutimiza idadi ya mchezaji wa 17 kuondoka klabuni Chelsea chini ya Antonio Conte katika kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili, sasa Antonio Conte anataka wa kuziba nafasi ya mserbia huyo kikosini.

Mpaka sasa kwa taarifa zilizopo ni kwamba Chelsea inamtaka kiungo wa Leicester city, Danny Drinkwater raia wa Uingereza.

Drinkwater mwenye miaka 27 ameingia kwenye hesabu za Chelsea mara baada ya Chelsea kumuuza Nemanja Matic kwenda Man utd kwa dau la paundi milioni 40. Na sasa imebakiwa na viungo watatu ambao wana uhakika kikosi cha kwanza ni wawili Cesc Fabregas na N'golo Kante huku Tiemoue Bakayoko akiwa nje akiuguza majeraha yake.

Drinkwater aliiongoza Leicester city kutwaa taji la ligi kuu Uingereza msimu wa 2015-2016 ambapo katika nafasi ya kiungo alicheza sambamba na N'golo Kante ambaye kwa sasa yupo Chelsea. Lakini baada ya kuisaidia Leicester kutwaa taji hilo alisaini kuendelea kuwepo klabuni hapo kwa miaka 5 ina maana mkataba wake wa sasa ndani ya Leicester unaisha 2021, na Chelsea inatajwa kumuwania ingawa inaonekana kocha wa Leicester, Shakespeare hana mpango wa kumuuza.

Lakini pia Chelsea inatajwa kuwawania Oxlade Chamberlain wa Arsenal ambaye katika mkataba wake amebakiza mwaka 1 na Ross Barkley wa Everton naye anatajwa kuwaniwa na Antonio Conte naye pia kabakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.