Nyota wa Serbia ambaye leo amejiunga rasmi na Manchester united akitokea Chelsea, Nemanja Matic ametumia mahojiano yake ya kwanza aliyofanya na waandishi wa habari akiwa kama mchezaji rasmi wa Man utd kuishukuru klabu yake ya zamani, Chelsea.
Nemanja Matic alisajiliwa na Chelsea mwaka 2009 na mwaka uliofuata alifanyiwa mabadilishano akipelekwa Benfica huku David Luiz akija Chelsea.
Miaka minne baadae yaani 2014 alisajiliwa tena na Chelsea kwa dau la paundi milioni 21 ambapo alisajiliwa na Jose Mourinho na kufanikiwa kutwaa kombe la ligi kuu Uingereza akiwa na kocha huyo, na kwa msimu huo Nemanja Matic alikuwa ndie kiungo aliyezuia mashambulizi mengi kuliko kiungo yoyote.
Sasa Mourinho ni mwalimu wa Man utd na ameamua kumsajili mchezaji huyo anayetengeneza idadi ya wachezaji watatu wakubwa kusajiliwa na kocha huyo katika dirisha hili kubwa la usajili.
Akiwa na Chelsea ametwaa mataji manne yaani ya ligi kuu mara 2, kombe la FA mara moja na kombe la ligi mara moja.
No comments:
Post a Comment