Chelsea bado inaangaika kutafuta saini za wachezaji wengine ambapo mpaka sasa inaripotiwa inafukuzia nyota atakayecheza upande wa Victor Moses na Marcos Alonso ambao wao wanacheza kama mawinga ambao muda wa kushambuliwa wanarudi na kuwa kama walinzi wa pembeni.
Kwa upande anaocheza Victor Moses ambaye anacheza kama "right wing back" yaani winga wa kulia anayekaba kuna kinda anafukuziwa kusaidina na Moses katika namba hiyo.
Kinda wa Valencia, Joao Cancelo mwenye miaka 21 anatajwa kufukuziwa na Chelsea ili kumpa changamoto Moses ambaye anaonekana kukosa upinzani na ata mtu wa kushindana naye kucheza upande huo.
Cancelo anaelezwa kama moja kati ya walinzi bora wa kulia akiichezea klabu ya Valencia ya nchini Hispania huku uraia wake ukiwa ni Ureno aliichezea Ureno chini ya miaka 21 katika mashindano ya kimataifa ya Ulaya na huko inaelezwa walitumwa maskauti wa Chelsea kwenda kumwangalia. Na sasa anatajwa kutakiwa na Chelsea.

No comments:
Post a Comment