Nahodha wa Chelsea, Gary Cahill ametoa neno juu ya mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa anayetazamiwa kuachana na klabu hiyo muda mfupi kuanzia sasa.
Gary Cahill alisema "Chelsea tutakumbuka mambo mengi kutoka kwa Diego [Costa] kuanzia katika ufungaji wa magoli mpaka tabia yake katika vyumba vya kubadilishia nguo"
Gary Cahill amechaguliwa kuwa nahodha wa tatu toka klabu hiyo kumilikiwa na Roman Abramovich na alikabidhiwa kitambaa hicho mara baada ya John Terry kuachana na klabu hiyo yenye makazi yake magharibi mwa London.
"Diego Costa atabaki kuwa Diego Costa. Huo ndio ukweli na hakika Chelsea itaukumbuka mchango wake kuanzia uwanjani mpaka vyumbani" alisema Cahill.
Lakini pia alitoa neno juu ya mshambuliaji aliyesajiliwa na Chelsea akitokea Real Madrid na kuwa mchezaji ghali zaidi kikosini hapo, Alvaro Morata. Cahill alisema "Ni mchezaji mzuri na bado anakuwa, anatakiwa kupambana kuongeza ubora wake lakini bado Chelsea itakumbuka huduma ya Diego Costa"

No comments:
Post a Comment