Baada ya mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal jumapili iliyopita, mashabiki wengi wa Chelsea kuomba Costa arudishwe kikosini, kocha wa timu hiyo Antonio Conte alitoa neno juu ya maombi hayo ya mashabiki.
Kocha Antonio Conte alisema "Nafikiri hivyo pia, lakini nadhani hili nilishalitolea maelezo tayari, na sioni haja ya kurudia nilichokisema"
Alisema kocha huyo alipofanyiwa mahojiano na chombo cha habari cha Sky Sports kwamba kumrudisha Diego Costa kikosini ni jambo ambalo haliwezekani kama alivyosema kabla kwenye mkutano wa waandishi wa habari na kocha huyo aliposema, ni wazi timu inajua, Costa mwenyewe anajua kwamba kinachotakiwa ni kuongea na wakala wake amtafutie timu nyengine ili imsajili.
Mapema mwezi wa sita wakati msimu ulipoisha na wachezaji wakiwa mapumzikoni kocha Antonio Conte alimtumia ujumbe Diego Costa na kumwambia hamuitaji tena kikosini na afanye jitihada atafute timu ya kucheza msimu ujao.

No comments:
Post a Comment