Kocha Antonio Conte anaonekana kukata tamaa juu ya usajili wa Alex Sandro kutokea Juventus, na sasa amemgeukia nyota mwenye sifa ya mlinzi mwenye kasi anayeichezea Tottenham, Danny Rose.
Rose anatakiwa na Chelsea na kuna taarifa zinasema klabu hiyo ina mpango wa kutoa paundi milioni 40 ili kumsajili nyota huyo mwenye uraia wa Uingereza.
Rose aliyecheza kwa mafanikio sana chini ya kikosi cha Tottenham kilichoipa usumbufu sana Chelsea msimu uliopita ikimaliza nyuma ya Chelsea anatakiwa pia na klabu ya Man utd.

No comments:
Post a Comment